Thursday 7 November 2013

HAYA NI MAENDELEO, SIKU HIZI KWENDA KLINIKI NI KUSINDIKIZANA BAINA YA MWANAMKE NA MWANAUME

MMOJA wa wanaume akimsindikiza mke wake kurudi nyumbani baada ya kupatiwa huduma ya Kliniki katika zahanati ya Kijiji cha Matongo Halmashauri ya Wilaya Ikungi, Tabia ambayo inabidi wanaume wote kuiiga ili kujua maendeleo ya mama na mtoto aliyopo tumboni. PICHA ya pili, baadhi ya wauguzi, mganga kiongozi wa zahanati hiyo, mtendaji wa kijiji na mmoja wa wananchi wa kijiji cha Matongo wakiwa kwenye picha ya pamoja nje ya zahanati hiyo , wakionyesha mshikamano wao katika masuala mbalimbali ya afya.
BAADHI ya wauguzi, mganga kiongozi wa zahanati hiyo, mtendaji wa kijiji na mmoja wa wananchi wa kijiji cha Matongo wakiwa kwenye picha ya pamoja nje ya zahanati hiyo , wakionyesha mshikamano wao katika masuala mbalimbali ya afya.

MKURUGENZI MANISPAA SINGIDA JOSEPH MCHINA AWEKA MKAKATI KUUWEKA MJI KATIKA HALI YA USAFI...

MKURUGENZI wa Manispaa Singida Joseph Mchina,akizungmuza na viongozi wa mitaa (hawapo kwenye picha) kuomba ushirikiano kwa ajili ya kuuweka mji katika hali ya usafi, hiyo ilifanyika wakati wa kikao maalumu cha kutambuana siku ya uzinduzi wa mabaraza ya usafi, iliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha maendeleo mjini Singida.
MCHUMI wa Manispaa Singida akiwasisitiza jambo wadau wa usafi wa katika mji wa Singida (hawapo pichani) wakati wa kikao maalumu cha kutambuana na kusisitza juu ya mipango ya Manispaa hiyo katika kuuweka mji safi, hiyo ilifanyika katika ukumbi wa chuo cha maendeleo mjini Singida. PICHA nyingine ya katikati ni mmoja wa wadau wa usafi akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Na Elisante John-IBAGA. WASANII wa nyimbo za Injili wanayo nafasi kubwa ya kuboresha maisha yao kupitia nyimbo wanazorekodi na kuziuza kwenye soko la ndani na nje ya nchi, hali ambayo inaweza kuwaingizia kiwango kikubwa cha fedha. Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Mgana Msindai alipokuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa CD ya nyimbo za Injili, iliyorekodiwa na bendi ya AGAPE, inayomilikiwa na kanisa la TAG Ibaga, katika wilaya Mkalama Mkoani Singida, Siku ya Jumapili iliyopita (Novemba 04,2013) kwenye viwanja vya soko Kijiji cha Ibaga. Alisema kuwa, sanaa ya nyimbo imewanyanyua wengi kimaisha kutokana na nyimbo zake kupendwa na idadi kubwa ya watu, hali inayowalazimu wazinunue kwa wingi CD hizo ili baadaye wasikilize neno la Mungu wakiwa nyumbani. “Nawaombeni sana ninyi wasanii wa nyimbo za injili, ongezeni bidii na ubora wa nyimbo zenu ili baadaye mnufaike na kazi zenu…wengi wametajirika kutokana na nyinbo za Injili,”alisisitiza Msindai.

MAMLAKA YA MAPATO (TRA) MKOA SINGIDA YAZINDUA SIKU YA MLIPA KODI...

Elisante John MAMLAKA ya mapato (TRA) Mkoa wa Singida unatarajia kuongeza mapato yake mara mbili ya kiwango cha makusanyo ya kodi, kutoka Sh. Bilioni 4.1 mwaka huu na kufikia zaidi ya Sh. Bilioni 8.3 ifikapo mwaka 2017/18. Afisa elimu kwa mlipa kodi wa malaka hiyo Mkoa wa Singida, Zacharia Gwagilo alisema hayo, wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya saba, siku ya mlipa kodi kimkoa katika ofisi za TRA, mjini Singida. Alisema katika kusherehekea siku ya mlipa kodi TRA Singida inaadhimisha kwa kusaidia wodi ya wazazi katika hospitali ya wilaya Manyoni na Iramba, kutembelea kituo cha wasioona Sabasaba, kusaidia kituo cha watoto wenye ulemavu wa akili Siuyu na kufanya semina kwa makundi mbalimbali ya walipa kodi. Kwa mujibu wa Gwagilo, ujumbe wa siku ya mlipa kodi mwaka huu ni “TULIPE KODI KWA MATOKEO MAKUBWA SASA”.