Thursday 7 November 2013

Na Elisante John-IBAGA. WASANII wa nyimbo za Injili wanayo nafasi kubwa ya kuboresha maisha yao kupitia nyimbo wanazorekodi na kuziuza kwenye soko la ndani na nje ya nchi, hali ambayo inaweza kuwaingizia kiwango kikubwa cha fedha. Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Mgana Msindai alipokuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa CD ya nyimbo za Injili, iliyorekodiwa na bendi ya AGAPE, inayomilikiwa na kanisa la TAG Ibaga, katika wilaya Mkalama Mkoani Singida, Siku ya Jumapili iliyopita (Novemba 04,2013) kwenye viwanja vya soko Kijiji cha Ibaga. Alisema kuwa, sanaa ya nyimbo imewanyanyua wengi kimaisha kutokana na nyimbo zake kupendwa na idadi kubwa ya watu, hali inayowalazimu wazinunue kwa wingi CD hizo ili baadaye wasikilize neno la Mungu wakiwa nyumbani. “Nawaombeni sana ninyi wasanii wa nyimbo za injili, ongezeni bidii na ubora wa nyimbo zenu ili baadaye mnufaike na kazi zenu…wengi wametajirika kutokana na nyinbo za Injili,”alisisitiza Msindai.

No comments:

Post a Comment