Sunday 29 September 2013

WIKI YA NENDA KWA USALAMA ILIVYOKUWA SINGIDA JUMAPILI...

MRATIBU wa mamlaka ya usafiri nchi kavu na majini (SUMATRA) Mkoa Singida Bw. Daniel Chilongani akihutubia wananchi na wadau wa usafirishaji, katika sherehe zilizofanyika kwenye viwanja vya stendi ya Msufini jana katika kuadhimisha WIKI YA NENDA KWA USALAMA kimkoa zilizofanyika jana jumapili. KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Singida Geofrey Kamwela akizungmza na wananchi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika sherehe za WIKI YA NENDA KWA USALAMA Kimkoa zilizofanyika viwanja vya stendi ya Msufini mjini Singida. MMOJA wa askari akitoa maelekezo ya alama za barabarani mbele ya mgeni rasmi Daniel Chilongani ambaye ni mratibu wa SUMATRA Mkoa, katika sherehe za WIKI YA NENDA KWA USALAMA zilizofanyika kwenye viwanja vya stendi ya Msufini mjini Singida (wa pili kulia) ni kamanda wa polisi mkoani Singida, Geofrey Kamwela.

Saturday 28 September 2013

MWANAMKE ATUHUMIWA KUMUUA MJUKUU WAKE WA KIKE..

MAELEZO YA PICHA:Mwenyekiti Mtaa wa Lulumba New Kiomboi katika wilaya Iramba Bw. Abel Seith akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) juu ya kifo cha msichana Zuhura Alfred (6) kumwagiwa maji ya moto na mtu anayedaiwa kuwa bibi aliyetajwa kwa jina la Magreth Sombi (55) na kumsababishia mauti. PICHA YA MWANAMKE ALIYEFUNGA KICHWA KITAMBAA: Ni mtuhumiwa Magreth Sombi (55) anayedaiwa kuhusika na mauaji ya mjukuu wake (Zuhura) baada ya kummwagia maji ya moto aliyokuwa atumie kusongea ugali majira ya jioni. PICHA YA MSICHANA ALIYEVAA NYWELE BANDIA:Ni binti wa Magreth anayejulikana kwa jina la Naomi Sanga (20) anayedaiwa kushirikiana na mama yake mzazi katika mauaji ya mtoto Zuhura kwa kumwagia maji ya moto. Naomi amehitimu mafunzo ya ualimu mkoani Tabora hivi karibuni na anasubiri kupangiwa kituo cha kazi. Naomi na mama yake wanashikiliwa na Polisi wilayani Iramba juu ya mauaji hayo. Na Elisante John,Kiomboi-Iramba Septemba 28, 2013:MSICHANA aliyejulikana kwa jina moja la Zuhura Alfred (6) mkazi wa mtaa wa Lulumba-New Kiomboi wilaya Iramba mkoa wa Singida amefariki dunia kutokana na kile kilichoelezwa na wananchi kuwa kifo hicho kimetokana na kumwagiwa maji ya moto na bibi yake aliyetajwa kwa jina la Magreth Sombi (55). Mwanamke huyo alimmwagiwa motto maji hayo ambayo yalikuwa yatumike kusongea ugali majira ya jioni baada ya mtoto kuwa amechelewa kupeleka mwiko wa kupikia aliokuwa ametumwa kutoka kabatini. Akieleza kisa hicho Mwenyekiti wa mtaa huo Abel Seth Muna alisema tukio hilo lilitokea siku ya jumanne (septemba 24) mwaka huu majira ya jioni katika eneo wanaloishi, mtaa wa Lulumba-New Kiomboi. Alisema siku hiyo marehemu baada ya kuchelewa kuukabidhi mwiko huo kutoka alikotumwa, alimwagiwa maji ya moto yaliyokuwa yamechemka tayari kutumika kupikia ugali na kujeruhiwa vibaya katika sehemu kubwa ya mwili wake ikiwemo mikononi na miguuni kiasi cha nyama za mikononi kumomonyoka "Kama hiyo haikutosha, Magreth kwa kushirikiana na mwanae (Naomi) walimkamata kwa nguvu mtoto huyo na kutumbukiza viganja vyake vyote ndani ya sufuria lililokuwa na maji ya moto....mtoto aliungua sana hadi nyama zote za mkononi zikatoka...,"alisema kwa masikitiko. Mwenyekiti huyo alisema binti huyo alifariki dunia siku ya pili yake siku ya septemba 26 akipatiwa tiba katika hospitali ya wilaya ya Iramba, mjini Kiomboi. Alisema baada ya binti huyo kufariki Magreth alimtuma Naomi kwenda nyumbani kwa mwenyekiti kutoa taarifa juu ya kifo hicho huku akiacha kuwataarifu majirani zake waliomzunguka. "Nilipomhoji sababu ya kutowajulisha majirani zake, aliniomba nisiwaambie kwa sababu hataki watu wengi wajue au waje kurundikana kwake eti mwili wa Zuhura utachukuliwa na ndugu zake kwenda kuzika Singida mjini wakati wowote,"alisema kwa masikitiko Seth. Naye jirani mwingine wa karibu Elieza Mgwali alisema msichana huyo ambaye ana miezi miwili tangu aanze kuishi na bibi yake alikuwa na wakati mgumu kutokana na mateso aliyokuwa anapata kutoka kwa bibi yake (Magreth). "Mtoto ameteseka sana, alifanyishwa kazi nzito ambazo zipo nje ya uwezo wake na alikuwa ananyimwa mpaka chakula...alikuwa anakuja kwangu moja kwa moja anaingia jikoni kutafuta chakula, tulishatambua mateso yake hivyo tulikuwa tunamruhusu ale mpaka ashibe,"alisema Mgwali. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Geofrey Kamwela amekiri kuwepo kwa tukio hilo na amesema kuwa tayari Naomi na mama yake (Magreth) wanashikiliwa, tayari kupandishwa kizimbani wakati wowote. MWISHO.

Thursday 26 September 2013

afisa elimu taaluma...

MKUU WA MKOA SINGIDA DK.PARSEKO KONE AFUNGUA KIKAO CHA BODI YA BARABARA...

MKUU wa Mkoa Singida Dk. Parseko Kone akifungua kikao cha 35 Bodi ya barabara kilichofanyika kwenye ukumbi wa jengo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo. Kushoto kwake ni Mwenyekiti CCM Mkoa Mgana Msindai na kulia kwake ni Mbunge jimbo Singida Magharibi Mohammed Misanga, Katibu tawala wa Mkoa Liana Hassan na aliyesimama ni Bw. Mwatawala kutoka ofisi ya TAMISEMI Mkoa.

EMMANUEL MICHAEL AKIPATA MSOSI WA NGUVU...

Mwandishi wa habari Emmanuel Michael akipata chakula muda mfupi mara baada ya kumaliza ratiba ya nusu siku kwa mafunzo ya Online Journalism ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo yaliyofanyika Kiomboi mjini Wilayani Iramba na kuhudhuriwa na wanahabari 16 wa Mkoa wa Singida.

WAANDISHI WA HABARI KWA VITENDO...


Baadhi ya waandishi wa habari Mkoa wa Singida wakiwa kwenye mafunzo ya kompyuta yaliyofanyika mjini Kiomboi chini ya ufadhili wa Muungano wa Klabu za habari nchini (UTPC) na kusimamiwa na klabu ya habari Mkoa Singida. Kutoka kushoto ni mwanahabari Damiano Mkumbo, Elisante Mkumbo (mapicha), mkufunzi wa mafunzo hayo John Mnubi kutoka Iringa na wa mwisho ni Festo Sanga. 

M,WANDISHI WA HABARI NATHANIEL LIMU...


Mwanadishi wa habari Nathaniel Limu (kushoto) akiwa kwenye foleni ya kupata chakula wakati wa mafunzo ya Online Journalism yaliyofanyika mjini Kiomboi katika Wilaya ya Iramba kuanzia Septemba 23-26, 2013. wengine (wanawake wawili) ni wajasiriamali wa chakula waliokuwa wakihudumia waandishi hao kwa chakula.


Tuesday 24 September 2013

Dini chemchem ya amani....


        


  • NJOMBE CHUO 044 77775
Nazim Ansarullah wa jumuiya ya Ahmadiyya mkoa wa Iringa Bw Said Ahmad Ng'amilo akikabidhi vitabu vya Dini ya Kiislamu kwa Amir kiongozi wa wanafunzi wa kiislamu katika chuo cha maendeleo Njombe.(hd)



Monday 23 September 2013

Mmoja wa wanafunzi wa shule ya Msingi Gumanga akikabidhiwa cheti cha kuhitimu elimu ya Msingi mbele ya mgeni rasmi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Mgana Msindai, kwenye mahafali ya 16 ya shule hiyo.