Thursday 7 November 2013

HAYA NI MAENDELEO, SIKU HIZI KWENDA KLINIKI NI KUSINDIKIZANA BAINA YA MWANAMKE NA MWANAUME

MMOJA wa wanaume akimsindikiza mke wake kurudi nyumbani baada ya kupatiwa huduma ya Kliniki katika zahanati ya Kijiji cha Matongo Halmashauri ya Wilaya Ikungi, Tabia ambayo inabidi wanaume wote kuiiga ili kujua maendeleo ya mama na mtoto aliyopo tumboni. PICHA ya pili, baadhi ya wauguzi, mganga kiongozi wa zahanati hiyo, mtendaji wa kijiji na mmoja wa wananchi wa kijiji cha Matongo wakiwa kwenye picha ya pamoja nje ya zahanati hiyo , wakionyesha mshikamano wao katika masuala mbalimbali ya afya.
BAADHI ya wauguzi, mganga kiongozi wa zahanati hiyo, mtendaji wa kijiji na mmoja wa wananchi wa kijiji cha Matongo wakiwa kwenye picha ya pamoja nje ya zahanati hiyo , wakionyesha mshikamano wao katika masuala mbalimbali ya afya.

MKURUGENZI MANISPAA SINGIDA JOSEPH MCHINA AWEKA MKAKATI KUUWEKA MJI KATIKA HALI YA USAFI...

MKURUGENZI wa Manispaa Singida Joseph Mchina,akizungmuza na viongozi wa mitaa (hawapo kwenye picha) kuomba ushirikiano kwa ajili ya kuuweka mji katika hali ya usafi, hiyo ilifanyika wakati wa kikao maalumu cha kutambuana siku ya uzinduzi wa mabaraza ya usafi, iliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha maendeleo mjini Singida.
MCHUMI wa Manispaa Singida akiwasisitiza jambo wadau wa usafi wa katika mji wa Singida (hawapo pichani) wakati wa kikao maalumu cha kutambuana na kusisitza juu ya mipango ya Manispaa hiyo katika kuuweka mji safi, hiyo ilifanyika katika ukumbi wa chuo cha maendeleo mjini Singida. PICHA nyingine ya katikati ni mmoja wa wadau wa usafi akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Na Elisante John-IBAGA. WASANII wa nyimbo za Injili wanayo nafasi kubwa ya kuboresha maisha yao kupitia nyimbo wanazorekodi na kuziuza kwenye soko la ndani na nje ya nchi, hali ambayo inaweza kuwaingizia kiwango kikubwa cha fedha. Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Mgana Msindai alipokuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa CD ya nyimbo za Injili, iliyorekodiwa na bendi ya AGAPE, inayomilikiwa na kanisa la TAG Ibaga, katika wilaya Mkalama Mkoani Singida, Siku ya Jumapili iliyopita (Novemba 04,2013) kwenye viwanja vya soko Kijiji cha Ibaga. Alisema kuwa, sanaa ya nyimbo imewanyanyua wengi kimaisha kutokana na nyimbo zake kupendwa na idadi kubwa ya watu, hali inayowalazimu wazinunue kwa wingi CD hizo ili baadaye wasikilize neno la Mungu wakiwa nyumbani. “Nawaombeni sana ninyi wasanii wa nyimbo za injili, ongezeni bidii na ubora wa nyimbo zenu ili baadaye mnufaike na kazi zenu…wengi wametajirika kutokana na nyinbo za Injili,”alisisitiza Msindai.

MAMLAKA YA MAPATO (TRA) MKOA SINGIDA YAZINDUA SIKU YA MLIPA KODI...

Elisante John MAMLAKA ya mapato (TRA) Mkoa wa Singida unatarajia kuongeza mapato yake mara mbili ya kiwango cha makusanyo ya kodi, kutoka Sh. Bilioni 4.1 mwaka huu na kufikia zaidi ya Sh. Bilioni 8.3 ifikapo mwaka 2017/18. Afisa elimu kwa mlipa kodi wa malaka hiyo Mkoa wa Singida, Zacharia Gwagilo alisema hayo, wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya saba, siku ya mlipa kodi kimkoa katika ofisi za TRA, mjini Singida. Alisema katika kusherehekea siku ya mlipa kodi TRA Singida inaadhimisha kwa kusaidia wodi ya wazazi katika hospitali ya wilaya Manyoni na Iramba, kutembelea kituo cha wasioona Sabasaba, kusaidia kituo cha watoto wenye ulemavu wa akili Siuyu na kufanya semina kwa makundi mbalimbali ya walipa kodi. Kwa mujibu wa Gwagilo, ujumbe wa siku ya mlipa kodi mwaka huu ni “TULIPE KODI KWA MATOKEO MAKUBWA SASA”.

Saturday 19 October 2013

MAHAFALI YA TANO SHULE YA SEKONDARI KATA YA MWARU YAMEFANYIKA LEO SHULENI HAPO

SHULE ya kata Sekondari ya Mwaru iliyopo tarafa ya Sepuka Wilaya Ikungi imefanyika leo shuleni hapo ikitanguliwa na mgeni rasmi katika mahafali hayo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Mgana Msindai kuwakabidhi vyeti wanafunzi 11 wanaofanya mtihani mwaka huu kuhitimu kidato cha nne.


 
MMOJA wa wanafunzi wa Sekondari ya Mwaru iliyopo tarafa ya Sepuka Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida akipokea cheti kwa mgeni rasmi Mgana Msind Mwenyekiti wa CCM Mki ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Mkoani humo, katika sherehe za mahafali ya tano shuleni hapo leo. PICHA nyingine juu inawaonyesha wanafunzi kidato cha nne wakicheza muziki wa hiphop maarufu kwa jina la ‘Muziki wa kizazi kipya’ kama ishara ya kufurahia kumaliza miaka mine salama.


 SEHEMU ya madarasa ya shule ya Sekondari Mwaru iliyopo tarafa ya Sepuka Wilaya Ikungi Mkoani Singida.

BAADHI ya wazazi na walezi waliohudhuria sherehe hizo.

Thursday 17 October 2013

KAMBI YA UVCCM SINGIDA VIJIJINI ILIVYOFANA WAKATI WA UFUNGAJI ULIOFANYIKA KTK KATA YA KINYETO....

BAADHI ya vijana kutoka UVCCM Singida vijijini wakiwa ndani ya ukumbi katika makao makuu ya kata ya Kinyeto, tayari kumsikiliza mgeni rasmi Mwenyekiti wa CCM mkoa Singida Mgana Msindai (hayupo pichani). Ufungaji rasmi wa kambi hiyo umefanyika leo Oktoba 17,2013.
VIONGOZI mbalimbali wa CCM wakiwemo Makamanda wa UVCCM wa kata zote za Wilaya Singida Vijijini (waliovaa majoho) wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Singida Mgana Msindai, wan ne kutoka kushoto waliosimama, kabla ya kufunga kambi ya vijana iliyoendeshwa kwa siku saba kwenye kata ya Kinyeto. SEHEMU ya vijana, wake kwa waume wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi akifunga kambi hilo la siku saba, lililofanyika kijiji, kata ya Kinyeto Singida Vijijini.

KAMBI YA UVCCM SINGIDA VIJIJINI ILIYOFANYIKA KWA SIKU SABA KATIKA KATA KINYETO YAFUNGWA...

KUTOKA kulia,mtu wa pili ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa Wwa Singida, Mgana Msindai akiwa meza kuu kabla ya kufunga kambi ya wiki moja ili kufundwa juu ya mada mbalimbali, yaliyoandaliwa na Umoja wa Vijana CCM Singida Vijijini. Wa kwanza kulia ni mwenyekiti wa CCM Wilayani humo Narumba Hanje na kulia kwa Msindai ni Mwenyekiti wa UVCCM Singida vijijini Shabani Mang’ola.

Wednesday 16 October 2013

MWENYEKITI CCM MKOA SINGIDA MGANA MSINDAI AZINDUA TAWI LA HAILA KIJIJI CHA URUGHU WILAYANI IRAMBA...

MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Singida, Mgana Msindai Oktoba 16,2013 amefanya ziara katika kijiji cha Urughu Wilaya Iramba na kuzindua tawi jipya lililopo kitongoji cha Haila lenye wananchama zaidi ya 300 na baadaye kufanya mkutano eneo la makao makuu ya kata (Urughu), kabla ya mkutano huo wa hadhara ambapo wananchi walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali, mapema alikagua ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara sekondari ya Urughu na kukagua ujenzi wa kituo cha afya kinachojengwa kwa nguvu za wananchi wa kata hiyo na kuridhishwa sana na maendeleo ya ujenzi huo. Hata hivyo aliwasihi wananchi wa kata hiyo kuendelea kuchangia miradi ya maendeleo ili kuharakisha maendeleo kwenye eneo lao.

Wednesday 9 October 2013

WAANDISHI WA HABARI 20 KUTOKA SINGIDA, TABORA, DODOMA NA KIGOMA WAPEWA MAFUNZO JUU YA KUANDIKA HABARI ZA UKATILI DHIDI YA BINADAMU

MKUU wa Wilaya Bahi na Kaimu Mkuu wa Mkoa Dodoma, Betty Mkwasa akiwa na Deodatus Balile mkufunzi wa mafunzo kwa waandishi 20 wa habari juu ya kuandika kwa ufasaha taarifa za Ukatili wa kijinsia dhidi ya binadamu yaliyofanyika katika hotel ya Fifty six Mjini Dodoma. Hapa ni baada ya kuwa amefungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Dk. Rehema Nchimbi. WAANDISHI wa habari 20 kutoka mikoa ya Kigoma, Tabora, Singida na Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja na kaimu mkuu wa mkoa Dodoma Betty Mkwasa (katikati waliokaa kwenye viti), kulia ni mkufunzi wa mafunzo hayo Jamila na kushoto ni Balile.

Sunday 6 October 2013

SHEREHE ZA UWT ZILIVYOFANA WILAYA SINGIDA

SHEREHE ZA UWT WILAYA SINGIDA VIJIJINI ZILIVYOFANA NA KUHUDHURIWA NA MAELFU YA AKINA MAMA KUTOKA KONA ZOTE ZA WILAYA HIYO, AMBAZO ZILIHUTUBIWA NA MBUNGE WA JIMBO LA SINGIDA KASKAZINI LAZARO NYALANDU AMBAYE PIA NI NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII.

Tuesday 1 October 2013

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi (CCM) Manispaa Singida Janeth Nyakonji akimkaribisha mgeni rasmi mjumbe wa halmashauri kuu NEC-CCM taifa Singida mjini Hassan Mazala kufungua semina ya mafunzo kwa viongozi wa jumuiya hiyo.Kulia ni MNEC CCM Singida mjini Bw. Mazala. Mjumbe wa NEC-CCM Wilaya Singida mjini Hassan Mazala akifungua semina ya mafunzo ya siku mbili inayohudhuriwa na viongozi wa ngazi mbalimbali wa jumuiya ya wazazi wilaya Singida mjini. Wa kwanza kushoto na mjumbe wa halmashauri ya CCM Singida mjini Duda Mughenyi na anayefuata ni mwenyekiti jumuiya ya wazazi Bi. Janeth Nyakonji. Baadhi ya viongozi wa jumuiya ya wazazi (CCM) manispaa ya Singida wanaohudhuria semina hiyo kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha maendeleo ya wananchi (FDC), mjini Singida.

Sunday 29 September 2013

WIKI YA NENDA KWA USALAMA ILIVYOKUWA SINGIDA JUMAPILI...

MRATIBU wa mamlaka ya usafiri nchi kavu na majini (SUMATRA) Mkoa Singida Bw. Daniel Chilongani akihutubia wananchi na wadau wa usafirishaji, katika sherehe zilizofanyika kwenye viwanja vya stendi ya Msufini jana katika kuadhimisha WIKI YA NENDA KWA USALAMA kimkoa zilizofanyika jana jumapili. KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Singida Geofrey Kamwela akizungmza na wananchi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika sherehe za WIKI YA NENDA KWA USALAMA Kimkoa zilizofanyika viwanja vya stendi ya Msufini mjini Singida. MMOJA wa askari akitoa maelekezo ya alama za barabarani mbele ya mgeni rasmi Daniel Chilongani ambaye ni mratibu wa SUMATRA Mkoa, katika sherehe za WIKI YA NENDA KWA USALAMA zilizofanyika kwenye viwanja vya stendi ya Msufini mjini Singida (wa pili kulia) ni kamanda wa polisi mkoani Singida, Geofrey Kamwela.

Saturday 28 September 2013

MWANAMKE ATUHUMIWA KUMUUA MJUKUU WAKE WA KIKE..

MAELEZO YA PICHA:Mwenyekiti Mtaa wa Lulumba New Kiomboi katika wilaya Iramba Bw. Abel Seith akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) juu ya kifo cha msichana Zuhura Alfred (6) kumwagiwa maji ya moto na mtu anayedaiwa kuwa bibi aliyetajwa kwa jina la Magreth Sombi (55) na kumsababishia mauti. PICHA YA MWANAMKE ALIYEFUNGA KICHWA KITAMBAA: Ni mtuhumiwa Magreth Sombi (55) anayedaiwa kuhusika na mauaji ya mjukuu wake (Zuhura) baada ya kummwagia maji ya moto aliyokuwa atumie kusongea ugali majira ya jioni. PICHA YA MSICHANA ALIYEVAA NYWELE BANDIA:Ni binti wa Magreth anayejulikana kwa jina la Naomi Sanga (20) anayedaiwa kushirikiana na mama yake mzazi katika mauaji ya mtoto Zuhura kwa kumwagia maji ya moto. Naomi amehitimu mafunzo ya ualimu mkoani Tabora hivi karibuni na anasubiri kupangiwa kituo cha kazi. Naomi na mama yake wanashikiliwa na Polisi wilayani Iramba juu ya mauaji hayo. Na Elisante John,Kiomboi-Iramba Septemba 28, 2013:MSICHANA aliyejulikana kwa jina moja la Zuhura Alfred (6) mkazi wa mtaa wa Lulumba-New Kiomboi wilaya Iramba mkoa wa Singida amefariki dunia kutokana na kile kilichoelezwa na wananchi kuwa kifo hicho kimetokana na kumwagiwa maji ya moto na bibi yake aliyetajwa kwa jina la Magreth Sombi (55). Mwanamke huyo alimmwagiwa motto maji hayo ambayo yalikuwa yatumike kusongea ugali majira ya jioni baada ya mtoto kuwa amechelewa kupeleka mwiko wa kupikia aliokuwa ametumwa kutoka kabatini. Akieleza kisa hicho Mwenyekiti wa mtaa huo Abel Seth Muna alisema tukio hilo lilitokea siku ya jumanne (septemba 24) mwaka huu majira ya jioni katika eneo wanaloishi, mtaa wa Lulumba-New Kiomboi. Alisema siku hiyo marehemu baada ya kuchelewa kuukabidhi mwiko huo kutoka alikotumwa, alimwagiwa maji ya moto yaliyokuwa yamechemka tayari kutumika kupikia ugali na kujeruhiwa vibaya katika sehemu kubwa ya mwili wake ikiwemo mikononi na miguuni kiasi cha nyama za mikononi kumomonyoka "Kama hiyo haikutosha, Magreth kwa kushirikiana na mwanae (Naomi) walimkamata kwa nguvu mtoto huyo na kutumbukiza viganja vyake vyote ndani ya sufuria lililokuwa na maji ya moto....mtoto aliungua sana hadi nyama zote za mkononi zikatoka...,"alisema kwa masikitiko. Mwenyekiti huyo alisema binti huyo alifariki dunia siku ya pili yake siku ya septemba 26 akipatiwa tiba katika hospitali ya wilaya ya Iramba, mjini Kiomboi. Alisema baada ya binti huyo kufariki Magreth alimtuma Naomi kwenda nyumbani kwa mwenyekiti kutoa taarifa juu ya kifo hicho huku akiacha kuwataarifu majirani zake waliomzunguka. "Nilipomhoji sababu ya kutowajulisha majirani zake, aliniomba nisiwaambie kwa sababu hataki watu wengi wajue au waje kurundikana kwake eti mwili wa Zuhura utachukuliwa na ndugu zake kwenda kuzika Singida mjini wakati wowote,"alisema kwa masikitiko Seth. Naye jirani mwingine wa karibu Elieza Mgwali alisema msichana huyo ambaye ana miezi miwili tangu aanze kuishi na bibi yake alikuwa na wakati mgumu kutokana na mateso aliyokuwa anapata kutoka kwa bibi yake (Magreth). "Mtoto ameteseka sana, alifanyishwa kazi nzito ambazo zipo nje ya uwezo wake na alikuwa ananyimwa mpaka chakula...alikuwa anakuja kwangu moja kwa moja anaingia jikoni kutafuta chakula, tulishatambua mateso yake hivyo tulikuwa tunamruhusu ale mpaka ashibe,"alisema Mgwali. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Geofrey Kamwela amekiri kuwepo kwa tukio hilo na amesema kuwa tayari Naomi na mama yake (Magreth) wanashikiliwa, tayari kupandishwa kizimbani wakati wowote. MWISHO.